Taarifa Kuhusu Kipimo cha AR cha HUAWEI na Faragha

Ilisasishwa mara ya mwisho: Tarehe 26 Septemba 2022

Kipimo cha AR cha HUAWEI ni programu inayotolewa na Huawei Device Co., Ltd. (hapa ndani baadaye inarejelewa kama "Huawei", "nasi", "sisi", au "yetu") inayokuwezesha kupima miili ya binadamu na vitu katika ulimwengu halisi. Huawei huchukulia maelezo ya kibinafsi na faragha yako kimadhubuti na inajitolea kuchukua hatua mwafaka za usalama ili kulinda maelezo yako ya kibinafsi kulingana na sheria husika na viwango vya usalama vilivyowekwa vya sekta.

1 Jinsi Tunavyokusanya na Kutumia Maelezo Yako ya Kibinafsi

Tutakupa vipengele vilivyoelezwa hapo chini kupitia Kipimo cha AR cha HUAWEI. Ili kutimiza majukumu yetu ya kimkataba na kuhakikisha kuwa unaweza kutumia vipengele kama hivyo, tutasindika maelezo yanayohitajika ili kutoa vipengele kama ilivyoelezwa hapo chini unapovitumia. Usipotoa maelezo husika, matumizi yako ya vipengele katika programu hii yataathiriwa.

Kupima vitu na watu

Ili kupima urefu, kipimo cha eneo na ujazo wa kitu, pamoja na urefu wa watu, mpigo wa moyo na kasi ya kupumua (upatikanaji wa vipengele unaweza kutofautiana kulingana na modeli ya kifaa), tunahitaji kusindika kindani mtiririko wa uhakiki wa kamera, maelezo ya kipima uchapuzi, maelezo ya jairoskopu, maelezo ya sensa ya mvuto wa ardhi, maelezo ya kipima nguvu za sumaku, maelezo ya sensa ya mwelekeo wa skrini, sifa za mfumo na modeli ya kifaa chako. Ukitumia Kipimo cha AR kunasa na kuhifadhi picha za skrini za vipimo, tutasindika na kuhifadhi picha zako za skrini ndani ya kifaa.

Aidha, Kipimo cha AR cha HUAWEI hukuruhusu kushiriki data ya kipimo cha kitu chako (ikiwa ni pamoja na urefu, kipimo cha eneo na ujazo) na programu za watu wengine. Data haitaunganishwa na watu binafsi. Kabla ya kuzindua Kipimo cha AR cha HUAWEI kutoka kwa programu ya mtu mwingine, tafadhali soma sera ya faragha ya mtu huyo mwingine kwa makini.

2 Vibali Vinavyohitajika

Kamera: Kibali hiki kinahitajika ili tutambue miili ya binadamu na vitu katika ulimwengu halisi kwa kutumia algoriti za AR kupitia mtiririko wa uhakiki wa kamera unapotumia huduma za vipimo za programu hii. Usipotoa kibali hiki, hutaweza kutumia kipengele cha kipimo cha programu hii.

Hifadhi (au Midia na faili): Tunahitaji kibali hiki ili kunasa na kuhifadhi picha za skrini za vipimo unapogusa kitufe ili kuhifadhi matokeo ya kipimo. Ikiwa huhitaji huduma hii, unaweza kubatilisha kibali hiki wakati wowote. Matumizi yako ya huduma zingine hayatoathiriwa.

Unaweza kudhibiti vibali vya programu hii kutoka kwenye mipangilio ya mfumo.

3 Kuwasiliana Nasi

Tuna idara na wafanyakazi maalum kwa ajili ya kwa ulinzi wa maelezo ya kibinafsi. Unaweza kuwasiliana nasi kwa kutembelea ukurasa wa Maswali ya Faragha. Tutajibu haraka iwezekanavyo.

Ikiwa hujaridhishwa na jibu unalopokea, hasa ikiwa unahisi kuwa usindikaji wetu au tunavyoshughulikia maelezo yako ya kibinafsi kumekiuka au kuvunja haki na/au maslahi yako ya kisheria, unaweza kutafuta suluhisho kwingine, iwe ni kwa kuandikisha kesi kwenye mahakama ya watu ndani ya mamlaka husika, kuwasilisha lalamishi kwenye chama cha sekta kujidhibiti yenyewe au mashirika husika ya udhibiti ya serikali, au kwa mbinu zingine. Pia unaweza kushauriana nasi kuhusiana na njia zinazopatikana za kuwasilisha lalamishi lako.

Ukusanyaji na matumizi ya Huawei ya maelezo yako ya kibinafsi yanatawaliwa na sera yetu ya faragha. Ili kupata maelezo zaidi, tafadhali rejelea Taarifa ya Faragha ya Biashara ya Mteja wa Huawei.